Alhamisi , 29th Dec , 2022

Gwiji wa soka wa zamani wa Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amefariki dunia leo Alhamisi Desemba 29 akiwa na umri wa miaka 82. 

Pele akiwa ameshikilia Kome la Dunia

Mtoto wake wa kike Kely Nascimento, amethibitisha kifo cha baba yake baada ya kuugua saratani ya utumbo mpana na kulazwa hospitalini ambako alikuwa akip[ata matibabu.

Pele ambaye alitajwa kama mchezaji bora wa karne ya 21, enzi za uchezaji wake alifanikiwa kushinda mataji matatu ya Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazil.

Pele ndiye mfungaji bora wa timu ya taifa ya Brazil akiwa na mabao 77 katika michezo 92 akilingana idadi hiyo ya magoli na Neymar Jr. 

Katika ngazi ya klabu, ndiye mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya Santos ya Brazil akiwa na mabao 643 katika michezo 659.

Katika enzi ya dhahabu kwa Santos, aliiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa bara la Amerika ya Kusini maarufu kama Copa Libertadores mwaka 1962 na 1963 pamoja na klabu bingwa ya dunia enzi hizo ikiitwa Kombe la Mabara mwaka 1962 na 1963.

Anatajwa kama mchezaji aliyefunga zaidi ya magoli elfu 1000 kwenye maisha yake ya soka.