Jumanne , 19th Sep , 2017

Beki wa kati wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand ametangaza rasmi kuingia kwenye mchezo wa ngumi na tayari ameshaanza mazoezi kwaajili ya kuingia ulingoni.

Muingereza huyo amethibitisha atafanya masumbwi kama bondia rasmi na sio kwasababu tu ya kufurahisha nafsi yake. Tayari Ferdinand amemtangaza mwalimu wake ambaye ni Richie Woodhall akiwa mwalimu mzoefu aliyewahi kufundisha mabingwa mbalimbali wa WBC uzito wa kati.

Rio ambaye amewahi kukutwa na kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni amesema kwasasa anaendelea kujiweka fiti ili aweze kupata leseni ya kuwa mwana masumbwi.

Ferdinand akiwa Manchester United alifanikiwa kutwaa ubingwa wa England mara 6 pamoja na UEFA mara moja na hivi sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka kwenye runinga.