Jumatano , 27th Jul , 2016

Mchezaji wa Uswisi katika mchezo wa tennis Roger Federer, ametangaza kujitoa kwenye michuano ya Olimpiki, kufuatia kuuguza majeraha ya goti, aliyoyapata mwanzoni mwa mwaka huu.

Mswisi Roger Federer, amejitoa katika Olympiki za mwaka huu, kufuatia maumivu ya goti aliyoyapata na kufanyiwa upasuaji mwezi Februari mwaka huu.

Mapumziko hayo ya Federer yatamfanya kuikosa michezo yote ya msimu wa mwaka huu, na kusema, anahitaji kujijenga upya iwapo anataka kuendelea na mchezo wake wa Tenisi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Federer, amesema anasikitika kwa kutoiwakilisha nchi yake ya Uswisi huko Brazil katika Olympiki, na anajisikia vibaya kupoteza muda wa msimu uliosalia.