Alhamisi , 18th Mei , 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amedai timu ya Serengeti Boys haijabuka tu kama baadhi ya watu wanavyofikilia bali serikali ndiyo imefanya jitihada zote mpaka leo hii kuwepo katika mashindano ya kimataifa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe

Mwakyembe amebainisha hayo baada ya kuulizwa swali la nyongeza na Mbunge Grace Kiwalu kwa kutaka kujua serikali imetenga kiasi gani kwa ajili ya kusaidia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys ili iweze kufanya vizuri katika mashindano yake na hatimaye kurudi na kombe nchini.

“Timu ya Serengeti  haijaibuka tu lakini tumeanza nayo miaka 3 iliyopita kwa kushindanisha vijana wa chini ya umri wa miaka 5 tukapata, tukapata timu bora, tumeilea hiyo timu na kuhakikisha kwamba inashiriki kwenye mashindano ya kimataifa kabla ya hizi mechi 22 ambayo haijapata kutokea toka historia ya nchi hi. Yote hii ni uwezeshaji na uwekezaji wa serikali…Figure kamili yaani kiasi gani tumetumia kama serikali tutaindaa na tutampa Mhe. Mbunge lakini imejitoa kwa hali na mali kuhakikisha timu hii inatuletea ushindi katika mashindano haya”. Alisema Mwakyembe