Alhamisi , 27th Nov , 2014

Chama cha Mchezo wa Magongo nchini THA, kimeiomba Serikali kurudisha viwanja walivyokuwa wakivilimiki hapo awali ili kuweza kuendeleza kukuza vipaji vya mchezo huo kwa vijana hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa THA, Abraham Sykes amesema walikuwa wakimiliki viwanja vitatu ambavyo ni Lugalo,Gymkhana na kimoja kilichokuwa Diamond Jubilee Serikali ilivichukua bila kugawa viwanja ambavyo vingetumika kwa ajili ya mchezo huo.

Sykes amesema wana lengo la kukuza michezo kwa vijana lakini uhaba wa viwanja unawafanya kushindwa kuendelea na zoezi hilo ambalo ni la muhimu kwa upande wao na nchi kwa ujumla.