Jumatano , 20th Oct , 2021

Kikosi cha Simba kitaingia kambini baada ya mazoezi ya leo jioni Oktoba 2021 tayari kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana utakaochezwa Jumapili Oktoba 24, 2021.

Kikosi cha Simba cha msimu wa mwaka huu 2021-22

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambapo tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia mitandao ya simu na viingilio vimeshatangazwa.

Baada ya kikosi kurejea kutoka nchini Botswana kilipopata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza, wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya kurejea mazoezini.

Wachezaji wawili tu mshambuliaji akiwamo Chris Mugalu na kiungo Pape Sakho hawatakuwa sehemu ya kikosi kitachoingia kambini kutokana na kuendelea kuuguza majeraha.

Katika mchezo huo Simba inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote na kama ikitokea imepoteza basi iwe bao moja na hapo watakuwa rasmi wametinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa Afrika.