Jumapili , 29th Nov , 2020

Kocha wa Simba SC Sven Vandenbroeck, amesema katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali leo dhidi ya Plateau United, wataanza mchezo kwa kuimarisha zaidi eneo la ulinzi.

Kocha wa Simba SC Sven Vandenbroeck

Sven ameeleza watafanya hivyo kwasababu hawana taarifa za wapinzani wao.

Aidha ameongeza kuwa wakiwashawasoma wapinzani wao wataangalia uimara na udhaifu wao upo eneo gani na baada ya hapo watajua cha kufanya.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo Novemba 29, 2020 kwenye mji wa Jos huko Abuja Nigeria, kuanzia saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.