Jumapili , 15th Jan , 2017

Kikosi cha Simba SC tayari kipo Morogoro baaada ya kuondoka leo mchana kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Jumatano.

Kikosi cha Simba

Ikitoka kulikosakosa Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa 1-0 na Azam FC katika fainali usiku wa Ijumaa Uwanja wa Amaan, Zanzibar bao pekee la kiungo Himid Mao Mkami kwa shuti kali, Simba itajaribu kuendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu Jumatano.

Kwa sasa, Wekundu hao wa Msimbazi ndiyo wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao 44 za mechi 18, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 40 za mechi 18 pia.