Jumanne , 15th Aug , 2017

Msemaji wa Simba Haji Manara amefunguka na kusema klabu ya  Simba haijafanya usajili kwa kufuru ya pesa za mfanya biashara Mohamed Dewji bali ni utaratibu uliopo miaka yote kwa ajili ya kutafuta wachezaji wazuri.

Akizijibu tuhuma kuhusu Klabu ya Simba kujiendesha kwa hasara huku ikijua wazi haina vyanzo vingine vya mapato, Manara amesema kuwa kwa Tanzania klabu karibu zote zinajiendesha kwa hasara.

"Hakuna Klabu isiyojiendesha kwa hasara hapa nchini hilo linajulikana na siyo kwa Simba tu. Tunafanya mipango mingi kwa ajili ya kujikwamua katika hili. Siyo kweli kwamba Simba imetumia gharama kubwa za usajili kwa kuwa kuna pesa za Dewji. Muda mrefu tumekuwa tukifanya usajili wa aina hii sasa sifahamu hayo maneno yametoka wapi" Manara.

Katika hatua nyingine Manara amekanusha minong'ono yakwamba Mfanyabiashara huyo akijitoa Simba itashindwa kusimama imara.