Alhamisi , 21st Oct , 2021

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amewakingia kifua wachezaji wake kwa kusema wanafaa kupewa heshima wanayostahili baada ya kucheza kwa kujituma na kupindua meza kwa kupata ushindi wa mabao 3-2 Atalanta.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer (kushoto) na Cristiano Ronaldo (Kuklia)

“Msiwadharau hawa wachezaji, wanacheza kwa ajili ya Manchester United na wanafahamu ni kwa jinsi gani wana bahati ya kuvaa jezi ya United. kwani zaidi ya vijana milioni wa kike na wakiume duniani wanatamani lakini hawajapata bahati ya kucheza United” Alisema Solskjaer.

Majibu ya mkufunzi huyo yamekuja baada ya kuulizwa swali na waandishi wa habari kwamba wachezaji wa United wanampambania asifukuzwe kazi na kupelekea kujitoa zaidi uwanjani.

Ushindi wa United umewapeleka kileleni mwa kundi F wakiwa na alama 6 huku Jumapili ya Oktoba 24, 2021 wakitaraji kuwa na kibarua kigumu dhidi ya Liverpool kwenye Epl.