Jumanne , 28th Mar , 2017

Kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kitakachoivaa Burundi katika mchezo wa kirafiki hii leo kimewekwa hadharani, huku kikionesha mabadiliko kadhaa katika baadhi ya idara ikilinganishwa na kile kilichoanza kuivaa Botswana siku ya Jumamosi.

Wachezaji wa Taifa Stars katika mazoezi

Katika kikosi cha leo, langoni anasimama Deogratius Munishi 'Dida' badala ya Aish Manula aliyeanza katika kikosi kilichopita huku katika nafasi ya ulinzi akiingia beki wa kati Salum Mbonde badala ya Erasto Nyoni ambaye alipigiwa kelele na mshabiki wa soka nchini kwa madai ya kutokuwa fiti.

Katika safu ya kiungo wa kati leo wataanza Himid Mao na Mzamiru Yasin ambapo Mzamiru anachukua nafasi ya Frank Domayo aliyenza katika kikosi kilichopita.

Viongo wa pembeni ni Farid Musa na Saimon Msuva, ambapo Farid amempumzisha Shiza Kichuya ambaye alionekana kutokuwa fiti katika mchezo uliopita.

Mwingine ambaye katika mchezo wa leo anaanza katika kikosi cha kwanza ni Salum Aboubakary, ambaye atakuwa msaidizi wa mshambuliaji pekee Ibrahim Ajibu. Salum anachukua nafasi ya Ajibu huku Ajibu akichukua nafasi ya nahodha Mbwana Samatta katika kikosi kilichopita.

Kikosi kamili hiki hapa