Jumatano , 26th Jul , 2017

Uongozi wa timu ya Tanzania Prisons umedai umefanya marekebisho makubwa katika kikosi chao kuelekea msimu mpya wa ligi kuu kwa kuwatema baadhi ya wachezaji waliyokuwa raia na badala yake sasa hivi watakuwa wanawachukua watu kutoka katika jeshi lao

 ili waweze kuwatumikia kwa kipindi kirefu.

Havintishi amebainisha hayo ikiwa zimebakia siku chache vumbi kuanza kutimuka katika michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2017/2018.

"Sasa hivi tunapunguza raia kutoka 10 mpaka watano,kikubwa tunachotaka tunachokifanya ni kutengeneza zaidi 'under 20' ndiyo ambayo itatupa dira ya mfumo wetu mzima wa timu. Kwa sababu mfumo wetu wa timu sasa tunataka tuwe tunawatumia askari wetu na raia tutabaki nao wachache kama wanne tu, sasa hivi tunatengeneza vijana ili watutumikie kwa muda mrefu zaidi", amesema Havintishi.

Pamoja na hayo, Havintishi amesema watambana wakiwa na wachezaji wao wenye chini ya umri wa miaka 20 bila ya kuwa na wasiwasi wa aina yoyote katika ligi kuu kwa sababu tayari wameshawajenga vizuri.

Kwa upande mwingine, Katibu huyo amewataja wachezaji ambao wametemwa katika kikosi hicho ni pamoja na Victor Hangaya ambapo katika msimu uliyopita aliweza kuwafunga Simba mabao 2 pamoja na Mohamed Samatta.