Ijumaa , 20th Jan , 2017

Hatimaye baada ya kusubiri kwa muda mrefu mshambuliaji wa kimataifa Thomas Ulimwengu amefanikiwa kupata timu nchini Sweden, Athletic Eskistuma, inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Thomas Ulimwengu

Meneja wa mchezaji huyo Jamal Kisongo amezungumza na kipenga na kuthibitisha juu ya taarifa hizo za Ulimwengu ambaye anatarajiwa kuondoka nchini mapema wiki ijayo ili kukamilisha mazungumzo na timu hiyo .

Wakati huo huo Jamal Kisongo ameiambia Kipenga kuwa amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kuanza kupotosha ukweli juu ya usajili wa mchezaji Thomas Ulimwengu wakimshutumu kumshauri vibaya mchezaji huyo

Akizungumza hii leo, Ulimwengu amesema kwamba baada ya mazungumzo ya awali na klabu hiyo anakwenda kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama FC Cafe Opera na Vasby United..

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa watu wangu wote wa karibu kama Jamal Kisongo ambao wamekuwa karibu na mimi kwa kipindi chote hiki na kunipa ushauri hadi kufikia maamuzi haya ya kujiunga na timu hii. Tumekataa ofa nyingi sana na kuikubali hii kwa sababu za msingi sana,” alisema.

Kwa upande wa meneja wake, Jama Kisongo, amesema masuala ya mkataba wa mchezaji huyo bado hayajakamilika, na kwamba akifika takamilisha kila kitu.

Msikilize hapa akifanya mahojiano na kipindi cha Kipenga cha EA Radio........

Sauti ya Jamal Kisongo