Jumanne , 22nd Jul , 2014

Timu ya taifa ya vijana wa umri chini ya miaka 18 ya Tanzania mchezo wa cricket imeendelea na mazoezi mazito katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam ili kujiwinda na michuano ya Afrika kusaka tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia

Wachezaji wa timu ya vijana ya cricket ya Tanzania wakijifua jijini Dar es salaam

Wachezaji 14 na viongozi 3 wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 18 ya Tanzania mchezo wa cricket wanataraji kuondoka nchini August 7 mwaka huu kwenda jijini Lusaka Zambia kwenda kushiriki michuano ya Afrika kanda ya tano kwa ajili ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya dunia itakayofanyika mwakani nchini Singapore

Kocha mkuu wa timu hiyo ambayo inafanya mazoezi katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es salaam sehemu ya mlimani Hamis Abdalah amesema vijana wake wako tayari na wana morali ya hali ya juu kitu ambacho kinampa matumaini ya kufanya vema katika michuano hiyo itakayoanza August 9 mwaka huu huko jijini Lusaka Zambia.