Jumanne , 17th Jan , 2017

Kocha wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya Uholanzi Louis van Gaal ametangaza kustaafu kufundisha soka baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 26.

Louis Van Gaal

Van Gaal, mwenye umri wa miaka 65, amekuwa nje ya kazi tangu atemwe na Manchester United, mwezi Mei mwaka 2016.

Van Gaal, alitangaza kujitoa wakati akipokea tuzo ya mafanikio ya muda mrefu, iliyotolewa na Serikali ya Uholanzi, kumpa heshima yake ya mchango wake kwenye mpira wa miguu.

Van Gaal amechukua mataji ya ligi na vilabu vya Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Ajax (1994-95) na Uefa Cup: Ajax (1991-92), pamoja na FA Cup: Manchester United (2015-16)