Jumatano , 27th Jul , 2016

Kama umeshawahi kumuona mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil, Ronaldo de Lima akisumbuka kupunguza ubonge ili achezea mpira kama alivyoanza, na mwishowe akashindwa, basi hiyo inaweza kutokea pia katika kikosi cha Man City.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji wake kula hovyo na kuongezeka uzito na tayari ameshampa marufuku kiungo Samir Nasri.

Mlinzi wa timu hiyo, Gael Clichy amesema Mhisapnia huyo amewazuia kula, pizza, juice, na vyakula vya kuongeza uzito.

Clichy amesema, kama mchezaji uzito wake ni kilo 60, halafu anazidi hadi kilo 70, basi anakuwa hawezi kucheza mpira, ambapo Nasri, ameambiwa kupunguza uzito.