Jumatano , 22nd Oct , 2014

Nahodha wa Klabu ya Gofu ya Lugalo,Japhet Masai amesema watanzania wanaojiamini na wenye uwezo wa kucheza mchezo wa Gofu wanatakiwa kujitokeza katika mashindano ya wazi ya mchezo huo yanayotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.

Akizungumza na East Afrika Radio, Masai amesema mashindano hayo ambayo ni makubwa na yenye kuchagua mchezaji wa mwaka yatasaidia kuweza kukuza na kupata vipaji vipya kwa vijana na hata wachezaji wenye umri mkubwa watakaoweza kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Masai amesema michuano hiyo mara nyingi hufanyika Dar es salaam kutokana na urahisi wa upatikanaji wa vifaa vya michezo ambapo kwa baadhi ya mikoa hapa nchini ni vigumu kuvipata.