Ijumaa , 23rd Jun , 2017

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara (aliyefungiwa), amefungukia kitendo cha mashabiki wa Yanga kuchoma jezi ya mchezaji wao kwa kusema hawana ustaarabu hata kidogo huku akiwapiga kijembe kwamba wajiandae kuchoma nyingine.

Manara amebainisha hayo kupitia mtandao wake wa kijamii siku moja kupita tokea kwa mashabiki kindaki ndaki wa klabu ya Yanga walioonekana wakichoma moto jezi aliyokuwa akivaa  Nahodha wao Haruna Niyonzima kabla ya kushindwana, kitendo kilichowatia hasira mashabiki hao.

"Katika miaka ya karibuni wachezaji kadhaa wa Simba walihamia Gongowazi hazikuchomwa moto jezi zao, wenzetu ustaarabu ziro ila wajiandae kuchoma nyingine 'soon' kama mlivyofanya mtafanyiwa 'the same" aliandika Manara