Jumatano , 26th Jul , 2017

Jumla ya wachezaji 20 wa kikosi cha pili cha Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga chini ya kocha Shadrack Nsajigwa wamesafiri asubuhi ya leo kuelekea jijini Mbeya tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Mbeya City FC ya mkoani humo.

kocha Shadrack Nsajigwa.

Hayo yameweka bayana na msemaji wa klabu hiyo Dismas Ten katika taarifa yake aliyoitoa leo na kusema mchezo huo wa hisani umeandaliwa na Tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) iliyo chini ya ofisi ya waziri mkuu utapigwa kesho Alhamis katika dimba la Sokoine jijini humo.

Pamoja na hayo, Ten  amesema kikosi hicho kitarejea jijini Dar es Salaam mara baada ya mchezo huo kuchezwa huku akisisitiza kuwa kikosi hicho siyo cha vijana wenye umri chini ya miaka 20, bali ni kikosi cha pili.