Jumatano , 17th Mei , 2017

Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini, SportPesa leo imeingia mkataba wa udhamini na klabu ya Yanga SC wenye thamani ya Shilingi billioni 5.22 kwa kipindi cha miaka mitano zaidi ya mahasimu wao , wekundu wa Msimbazi Simba SC.

Yanga inakua ni klabu ya pili nchini kulamba udhamini huo ikiwa ni baada ya watani wao wajadi Simba kufanya hivyo juma moja kupita kwa dau la Shilingi Bilioni 4.96.

Akizungumza wakati hafla ya kusaini mkataba huo makao makuu ya Yanga, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas  amesema wameingia udhamini na klabu hiyo kwa dhumuni la kuendeleza soka katika kufikia malengo waliyojiwekea.

"Fedha hizo zitatolewa kwa awamu, mwaka wa kwanza, Yanga watapata Sh. Milioni 950 na kama ilivyo kwa Simba, klabu ya Jangwani pia itatakiwa kuthibitisha matumizi ya fedha hizo kama yamefanyika kwa shughuli za maendeleo ya soka...Pia ikishinda michuano kama Kagame watapewa zawadi na wakifanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika watapata zawadi ya Mili. 250". Alisema Tarimba

Kwa mara nyingine tena, mahasimu hao wa jadi Simba na Yanga wanatarajiwa kuwa chini ya udhamini mmoja tena