Jumapili , 21st Mei , 2017

Wachezaji wa klabu ya Yanga wameonekana kujawa na furaha sana baada ya kuchukua ubingwa kwa mara ya 3 mfululizo ikiwa ni ubingwa wa 27 tangu klabu hiyo kuanzishwa mwaka 1935.

Saimon Msuva (Kushoto) na Thaban Kamusoko.

Yanga walikabindhiwa kombe la ushindi jana Jijini Mwanza baada ya mechi dhidi ya Mbao FC licha ya kuwa Mbao waliwafunga goli 1-0.

Baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wametoa shukrani kwa mashabiki na kwa watu wote ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa pamoja na kuchangia mafanikio hayo katika msimu huu.

"Naishiwa maneno ila najua nguvu kubwa ni nyinyi Mashabiki zetu, Asanteni na Hongereni Pia Kwa Ubingwa pamoja we can" - Saimon Msuva.

"Katika maisha yangu ya mpira, namshukuru Mungu kwani nimeweza kucheza Tanzania misimu 6, na nimeweza kuchukua ubingwa mara 4, ila nimechukua ubingwa mara 3 mfululizo" - Haruna Niyonzima

"YANGA 27 TIMES CHAMPIONS" - Thaban Kamusoko.

"It has been a long journey thank you all especially for all u done for me" - Donald Ngoma.

Yanga wameshawasili Jiji Dar es Salaam, ni sherehe na furaha zinaendelea Jangwani.