Jumatatu , 22nd Mei , 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini, ZuberI Zitto Kabwe amewatia moyo timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys huku akiwapongeza kwa kazi kubwa waliyoifanya kuitambulisha nchi katika soka la kimataifa.

Zitto amesema hayo baada ya timu hiyo kuondolewa rasmi kwenye hatua ya makundi ya kuwania taji la Afrika kwa vijana nchini Gabon kwa kufungwa  bao 1-0 na Niger mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.

"Vijana wetu wa Serengeti Boys mmefanya kazi kubwa kutambulisha nchi yetu kwenye soka la kimataifa...Ni wajibu wetu kuwaendeleza kivipaji na kusonga mbele, kutoka mashindanoni ni sehemu ya mashindano. Tuangalie mbele, hongereni sana". Aliandika Zitto kupitia ukurasa wake wa kijamii facebook