Jumapili , 15th Jan , 2017

Wakati United  ikijianda kuivaa Liverpool leo saa moja jioni, mshambuliaji wake mwenye maajabu Ibra Magic raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amesisitiza kuwa Manchester United bado inaweza kutwaa ubingwa Ligi Kuu Uingereza msimu huu.

Zlatan Ibrahimovic

 

Man United imehaha kuendeleza kiwango bora katika hatua za awali msimu huu, lakini mashetani hao wekundu wameshinda mechi tisa mfululizo katika michuano yote, sita zikiwa ni Ligi Kuu.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho bado kipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi lakini wamepunguza pengo la pointi dhidi ya vinara Chelsea hadi kufika pointi 10 na Ibrahimovic anaamini timu yake inaweza kupambana kutwaa ubingwa wa ligi iwapo wataifunga Liverpool katika uwanja wa Old Trafford siku ya leo.

"Ligi haitabiriki. Hakuna timu ambayo unaweza kusema itashinda na ikafanya hivyo," Ibrahimovic alikiambia Sky Sports News. "Chelsea imekuwa ikifanya vizuri, wanacheza mara moja kwa wiki, wana hali nzuri na nguvu nyingi kila wanapocheza, lakini walikuwa na wakati mgumu mwanzoni lakini walizinduka.

"Kama tutapanda pale na kuwasumbua, kila timu ina kipindi chake cha mafanikio. tumekuwa na wakati mzuri, tukishinda, tukipoteza na sasa tunashinda tena. Natumai tutaendelea hivyo na tunasubiri wengine wafanye makosa.

"Jumapili ni fursa nyingine ya kuchukua pointi kutoka nne bora. Kama tunaweza kuanza vita dhidi ya timu zilizo kwenye nne bora, baada ya kupoteza pointi nyingi ambazo hatukupaswa kuzikosa. Pengo limekuwa dogo sasa, na pointi hizo tunaweza kuanza kuzichukua kwa Liverpool,"

Ibrahimovic ambaye alitua Old Trafford kwa uhamisho huru amefunga magoli 18 katika michuano yote akiwa United, ikiwa ni pamoja na magoli 13 ya ligi