Sports in brief
Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limesema linasubiri taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na Chama Cha Soka nchini Misri (EFA) kuhusu hali ya usalama nchini Misri.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akizungumza jana, alisema wanaamini CAF na EFA watakuwa wanafuatilia kwa makini hali ya usalama ndani ya Misri na kama wataona hali bado ni tete ni wazi watawajulisha nini cha kufanya.
Yanga ya Dar es Salaam itacheza na Zamalek ya Misri katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika mwanzoni mwa mwezi ujao jijini Cairo, misri ambao mechi ya kwanza baina ya timu hizo itafanyika jijini Dar es Salaam Machi 18 mwaka huu.
Print
More Sports in Brief
Prime Time
EATV Shows