Sports in brief
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Jumatano watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika muendelezo wa mechi za Ligi Kuu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, mechi hiyo namba 112 itaanza saa 10.30 jioni. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute huku Yanga ikiwania kurejea kwenye nafasi yake ya pili katika msimamo badaa ya kushushwa na Azam.
Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31 nyuma ya Azam iliyo nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 32. Simba ndio inaongoza ikiwa na pointi 34. Kwa upande wa Mtibwa Sugar iko nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 22.
Mtibwa Sugar inaikabili Yanga ikiwa na mgogoro kwenye kikosi chake baada ya hivi karibuni uongozi kumsimamisha kwa muda usiojulikana kocha msaidizi Mecky Maxime, baada ya baadhi ya wachezaji kulalamika kuwa kocha huyo aliyedumu na Mtibwa Sugar kwa miaka 17, anawahujumu.
Print
More Sports in Brief
Prime Time
EATV Shows