Sports in brief
Yanga imegoma kuipa nafasi Simba kutawala kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya jana kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 katika mchezo wa ligi hiyo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na ushindi huo,Yanga imefikisha pointi 37 sawa na Simba inayoongoza ligi hiyo, lakini Simba ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga, ambapo ina faida ya mabao 17 wakati Yanga inayo 16, hivyo kuendelea kushika nafasi ya pili.
Simba ilifanikiwa kurejea kileleni juzi baada ya kuifunga Azam mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32. Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa dakika ya 47 na Davies Mwape aliyepiga shuti lililogonga mwamba wa juu na kutinga nyavuni, baada ya kupokea pasi ya Haruna Niyonzima.
Print
More Sports in Brief
Prime Time
EATV Shows