Sports in brief
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeishusha daraja timu ya AFC Arusha kutokana na kushindwa kutokea uwanjani.
AFC ya Arusha ilishindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya 94 KJ iliyokuwa ichezwe juzi kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 21 ya ligi hiyo timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi Ligi ya Taifa na matokeo ya michezo yake yote itafutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye mashindano.
Print
More Sports in Brief
Prime Time
EATV Shows