wasanii kutoka Arusha walaani vikali mauaji ya visu mkoani humo, wakizungumza na planet bongo wasanii hao wamesema tabia hiyo sasa imekithiri na kuzidi kuleta madhara mengi ikiwepo kupoteza nguvukazi na mengine yanayo fanana na hayo.
Historia inaonyesha kati ya waliopatwa na majanga hayo ni pamoja na Father Nelly wa kundi la X-plastaz ambalo kwasasa limejiwekea makazi yake nje ya nchi, Pacha kutoka kundi la Watengwa lenye makazi yake Kijenge ya juu jijini Arusha, Mlostii na wengine wengine wengi akiwemo Lord Eyez ambaye kwa bahati nzuri mauti hayakumfika.
Kwasasa wasanii wo Arusha wameanzisha kampeni ya kupinga mauwaji ya visu inayotambulika kama "Arusha bila visu Inawezekana".
Print
Comments
Next On:
EATV Shows