Ijumaa , 18th Sep , 2020

Wafanyabiashara wa mawe ya urembo (Tarazo) ambayo hutumiwa katika kunakishi majengo mbali mbali walioko kawe beach jijini, Dar es salaam, wameiomba serikali kupitia wizara ya madini kupunguza gharama ya upatikanaji wa leseni ya biashara hiyo kwa kuwa  wanalazimika pia kulipa kodi,

Picha ya mfano wa Mawe ya Urembo.

pamoja na vibali vingine.

Watu wengi hupendelea kuyatumia mawe haya kama urembo katika ujenzi na mapambo kwenye maeneo mbalimbali jambo ambalo limechagiza kushamiri kwa biashara hiyo na kupelekea baadhi ya vijana wengi kujihusisha na biashara hiyo ambayo wanayotoa katika mikoa ya Tanga na Iringa.

Licha ya biashara hiyo kutajwa kuwa na baadhi ya changamoto lakini bado imeajiri vijana na kinamama ambao hujipatia riziki zao na kuendesha maisha ya kila siku huku wakishukuru serikali kwa kuwaacha katika eneo hilo kufanya biashara hiyo.

Aidha wamesema katika kikundi hicho ambacho kina zaidi ya vijana hamsini ambao wameunganisha mitaji wengine wakisafirisha huku Baadhi yao wakiponda kuziweka katika saizi tofauti kulingana na mahitaji ya wateja wao.