Kinondoni kutotoa vitambulisho kwa wafanyabiashara

Ijumaa , 17th Jul , 2020

Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam imesema haitatoa vitambulisho vya ujasiriamali kwa wafanyabiashara.

Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam imesema haitatoa vitambulisho vya ujasiriamali kwa wafanyabiashara waliopo masokoni kwa kuwa hao tayari wapo kwenye mfumo wa sheria za uendeshaji masoko katika manispaa hiyo.

Msemaji wa Manispaa ya Kinondoni Sebastiani Mhowera amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wafanyabiashara wa soko la Kawe kulalamikia kukosa vitambulisho hivyo kwa mwaka huu.

Amesema mwaka jana walifanya makosa kwa kutoa vitambulisho hivi hadi kwa wale wafanyabiashara waliopo kwenye masoko lakini kwa mwaka huu hatutarudia kosa hilo na badala yake watavitoa vitambulisho hivyo kwa wale tu wasio na maeneo rasmi.

Kwa upande waowafanyabiashara katika soko la Kawe wameiomba serikali kuwasaidia kuwapatia vitambulisho hivyo kwa kuwa sasa wanalazimika kulipa ushuru wa shilingi 15,000 kila mwezi..