Makundi mmbalimbali kunufaika na nanenane

Alhamisi , 30th Jul , 2020

Katika kuelekea kuanza kwa maonesho ya nanenane August mosi makundi ya wakulima,wafugaji na Uvuvi wameaswa kuyatumia kujifunza mbinu mpya za umwagiliaji Uvuvi na matumizi ya kilimo

Katika kuelekea kuanza kwa maonesho ya nanenane  August mosi makundi ya wakulima,wafugaji na Uvuvi wameaswa kuyatumia kujifunza mbinu mpya za umwagiliaji Uvuvi na matumizi ya kilimo Cha kisasa ili kujiongezea kipato hasa katika kipindi hiki ambacho Teknolojia imechukua nafasi kubwa.

Akitoa taarifa ya ushiriki  wa makundi hayo kwa Manispaa ya Ilala ikiwa ni Kanda ya mashariki ambayo hufanyika Morogoro bi Tabu Shaibu amesema kauli mbiu ya mwaka huu 2020 ni kwa Maendeleo ya kilimo mifugo, Uvuvi chagua Kiongozi bora.

Aidha amewataka kutumia fursa hiyo kuwachagua Viongozi watakaoweza kusimamia Sera za kilimo, Uvuvi na Mifugo ili kuweza kuifikia Tanzania yenye uchumi wa Kati.

"Tayari tupo kwenye uchumi wa kati tunasisitiza uwekezaji katika kilimo ila kabla ya yote tunahitaji viongozi wenye kusimamia sera hizo kufanya mapinduzi katika viwanda kupitia uzalishaji katika kilimo"

Mwaka 2019 Manispaa hiyo ya ilala iliongoza kwa ushindi wa jumla Kati ya manispaa zote zilizoshiriki maonesho hayo ya nanenane na kuwawezesha wakulima wengi kunufaika zaidi.ikiwemo ufugaji wa Nyuki