Jumanne , 18th Feb , 2020

Wafanyabiashara ambao wanatoa zao la Nyanya kutoka mikoani, wamefungukana na kusema sababu inayofanya nyanya kupanda bei ni kutokana na mvua kubwa zilizonyesha hali iliyopelekea mazao hayo kusombwa na maji.

Picha ya wafanyabiashara wanaouza Nyanya

Wakizungumza na kipindi cha Supa Breakfast  kutoka East Africa Radio, kinachoruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 asubuhi mpaka 4:00 asubuhi, wafanyabiashara hao wamesema suala la nyanya kupanda bei kwao wanaona ni Neema.

"Mvua kubwa zilizonyesha ndiyo zimesababisha mazao ya nyanya kusombwa na maji ya mafuriko, hali iliyopelekea nyanya kuoza mashambani na nyanya huwa haziendani na mvua ndiyo maana sasa hivi hazifiki mjini au zikifika zinaharibika njiani"  Wafanyabiashara wa Nyanya.

Pia wameendelea kusema kwa sasa hivi bei ya tenga moja la nyanya linauzwa Tsh 90,000, nyanya tatu ni shilingi 1000.