TFDA yatua kwa wauza Vipodozi

Jumamosi , 8th Sep , 2018

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), imesisitiza kuwa wafanya biashara wa Vipodozi nchini wasiofuaat sheria kwa kuuza vipodozi vilivyopigwa marufuku wataendelea kupoteza mitaji yao kwa kufirisiwa.

TFDA kwenye mkutanon wao leo na wauza vipodozi.

Akionge leo kwenye mkutano wa pamoja kati ya TFDA na wauza vipodozi wa Kariakoo jijini Dar es salaam, Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba, Vipodozi na Bidhaa Dawa, Bi Grace Shimwela amesema kwa mujibu wa Sheria, hairuhusiwi kuingiza vipodozi au bidhaa zinazodhibitiwa bila ya kusajiliwa na TFDA. 

''Kabla ya kuingiza bidhaa toka nje ya nchi,, hakikisha una kibali cha TFDA ili kuepusha kuingiza bidhaa ambazo si salama na bora ambazo zitaharibiwa au kurudishwa zilikotoka kwa gharama yako hivyo kupoteza mtaji'', amesema.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa za Dawa wa TFDA, Bw. Adonis Bitegeko, amewakumbusha wafanyabiashara wa vipodozi kuwa TFDA kama Taasisi ya Umma, ni rafiki kwa wafanyabiashara wote wakiwemo wa vipodozi hivyo wasisite kupata ushauri kabla ya kuanza biashara ili kuepusha hasara pindi inapobanika bidhaa zao hazina ubora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara hao, Bw. Martin Mbwana amesema wamechoka kukamatwa mara kwa mara na vipodozi vyenye sumu hivyo wanahitaji elimu ya namna ya kufanya biashara hiy kwa kuzingatia matakwa ya sheria.