Jumatatu , 13th Jan , 2020

Thamani ya mauzo na manunuzi ya hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam(DSE), imepanda hadi kufikia bilioni 2.04 kwa juma lililoishia Januari 10, 2020, ukilinganisha na shilingi milioni 408.10 kwa juma lililoishia Januari 3, 2019.

Akitoa taarifa ya mwenendo wa soko hilo, Meneja Miradi wa DSE Emmanuel Nyalali, amesema kuwa kaunta ya TBL iliongoza kwa kuchangia asilimia 98.20, ya thamani ya mauzo yote ya hisa, ikifuatiwa na CRDB iliyochangia kwa asilimia 1.48.

Aidha Thamani ya Soko la Hisa ilipanda kwa Shilingi bilioni 210, mpaka kufikia Trilioni 17.36, ukilinganisha na Shilingi Trilioni 17.15 kwa juma lililoishia Januari 3, 2020, kupanda kwa thamani ya soko kulichangiwa na kupanda kwa bei ya hisa katika kaunta za KCB, EABL na Jubileee.