Jumatatu , 24th Feb , 2020

kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, imeanza kuwalipa fidia wateja wake wote, kutokana na uwepo wa tatizo la intaneti lililokuwa limejitokeza siku ya jana.

Vodacom Tanzania.

Akitoa taarifa hiyo kupitia EATV&EA Radio Digital, leo Februari 24, 2020, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, amesema kuwa fidia hiyo itatolewa kwa haki na uwazi na itawafikia wateja wote walioathiriwa.

"Wapo wateja ambao watapa MB 300 na wengine 600, kwa wale ambao vifurushi vyao vilimalizika jana watapokea vifurushi vyao kwa mfumo wa MB, kwa wale ambao hununua vifurushi kila siku watapata nyongeza ya bure" amesema Rosalynn.

Aidha Rosalynn ameongeza kuwa,"Wale ambao walinunua vifurushi wakati tatizo hilo limetokea watarudishiwa kwa njia ya muda wa maongezi au kwa njia ya M-PESA hii inategemeana tu mteja alinunua kwa njia na pia watapata nyongeza ya kifurushi cha bure".