Ijumaa , 18th Sep , 2020

Baadhi ya vijana wabunifu hasa katika sekta ya ufinyanzi na uchongaji wa mitungi ya mapambo ya maua, ambao kwa sasa imeajiri vijana wengi wameziomba mamlaka zinazojihusisha nao kuboresha soko la ndani.

Eatv hii leo imetembelea katika eneo la Mbezi Africana, maarufu kama kwa makaranga  ambapo kwa mujibu wa vijana wanaojihusisha na shughuli za kubuni na kutengeneza bidhaa hizo za vyungu wameelezea kuwa licha ya wao kupambana bado wanakabiliwa na sera zisizo rafiki, uhaba wa mitaji, pamoja na kukosekana kwa masoko ya uhakika  licha ya biashara hiyo kuwa ndio msingi wa maisha yao.

Licha ya ubunifu wanaofanya kuonesha kuwa na thamani kubwa kwa wageni wanaoingia nchini umeonekana kupewa thamani ndogo na sekta husika zinazosimamia sanaa na wabunifu licha ya kujairi kundi kubwa la watu katika fani mbali mbali.

Wabunifu hao hutumia sementi, nondo kutengeneza mapambo hayo ambayo bei hupanda juu kulingana na bei halisi ya malighafi wanazotumia.