Wafanyabiashara Mbeya wakutana na Kamishna wa TRA

Jumanne , 4th Feb , 2020

Katika kuhakikisha wafanyabiashara wanapiga hatua na kuendelea kulipa kodi ipasavyo, Kamishna Mkuu wa TRA Dr. Edwin Mhede, amekuwa akizunguka mikoa mbalimbali kwaajili ya kukutana nao na kujadili mambo mbalimbali.

Kamishna Mkuu wa TRA Dr. Edwin Mhede

Katika mwendelezo wa ziara zake, Februari 3, 2020 Kamishna Mhede, alikutana na kuzungumza na wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya.

Taarifa ya Mamlaka hiyo ya mapato imeeleza kuwa katika mazungumzo hayo, Kamishna Mkuu wa TRA na Wafanyabiashara walijadili kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

Wakati huo huo TRA inaendelea na Kampeni yake maalum ya kuelimisha wananchi juu ya athari za magendo, Ukanda wa bahari ya Hindi kwa mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es salaam na Tanga.

Kampeni hiyo imeanza Februari 3 na itakwenda hadi Februari 11, 2020.