Rais mstaafu wa Peru ajipiga risasi

Jumatano , 17th Apr , 2019

Rais wa zamani wa Peru, Alan García amejipiga risasi mwenyewe, baada ya kugundua kuwa anatafutwa na jeshi la polisi nchini humo kwa kosa la kupokea rushwa.

Rais wa zamani wa Peru, Alan García.

García anatuhumiwa kwa kuchukua rushwa kutoka kampuni ya ujenzi wa Brazil Odebrecht, ambapo amekuwa akizikataa tuhuma hizo mara kwa mara.

Luis Gonzales Posada, ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa chama cha García, amesema hali yake ni mbaya, "hebu tumuombee Mungu kumpa nguvu," aliwaambia waandishi wa habari hospitali.

García ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1985 hadi 1990 na kurudi madarakani tena mwaka 2006 hadi 2011.

Taarifa zilizotolewa na wachunguzi zinadai kuwa, yeye alichukua rushwa kutoka Odebrecht wakati wa kipindi cha pili cha Urais ambapo Odebrecht amekubali kulipa karibu $ 30m (£ 23m) kama rushwa nchini Peru tangu 2004.