Jumamosi , 23rd Jun , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amekifungua kiwanda cha pombe kali cha Mati Super Brand cha mjini Babati kilichofungwa na Mkemia Mkuu wa Serikali huku akitaka akamatwe yeye, badala ya wamiliki wa kiwanda hicho. 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti

Mnyeti ameyasema hayo jana wakati akichukua uamuzi huo ambapo amefafanua kwamba hakubaliani na sababu zilizotolewa mpaka kiwanda hicho kufungwa 

Akitoa maelezo Mnyeti amesema mwekezaji huyo amefunga mitambo yake na kutoa ajira kwa wananchi, badala ya kupewa ushirikiano watendaji wanaohusika, wao ndiyo  wanamkwamisha kwa kukifunga kiwanda, ikiwa ni takribani miezi mitatu sasa.

"Bado kuna watu wanaandaa mazingira ya rushwa, yaani badala watumie hata siku tatu za kumshauri kitaalamu wanakimbilia kufunga kiwanda. Kuna baadhi ya watumishi wa Serikali wana ukiritimba mno, sasa mimi nakifungua kiwanda hiki halafu wakija wanikamate mimi," amesema.

Mkemia Mkuu wa Serikali alikifunga kiwanda hicho kwa maelezo kuwa kimekosa kibali cha kuidhinisha matumizi ya kemikali za kuzalisha pombe hizo Machi, 2018.