Jumamosi , 23rd Jun , 2018

Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kutokuwa wavumilivu kitendo kinachopelekea kushawishi watendaji wa mamlaka hiyo ili apatiwe huduma kwa haraka.

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NIDA, Rose Mdami,

Akizungumza na www.eatv.tv, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano NIDA, Rose Mdami amesema kuwa wananchi wachache ndio wamekuwa wakivuruga zoezi hilo kwa kushawishi watendaji na waendeshaji wa zoezi hilo ambao nao pia huwa sio waaminifu.

“Kwenye vituo vyetu vyote tumeandika rushwa ni adui wa haki, lakini cha kushangaza changamoto imekuwa kubwa kwa wananchi wanaodai kuwa wana haraka wamekuwa wakishawishi watendaji wetu”, amesema Mdami

Aidha Rose ameongeza kuwa zoezi linaloendelea sasa ni uhakiki na uchakataji wa taarifa za wananchi na hatua ya mwisho itakuwa ni uzalishaji na utoaji wa vitambulisho hivyo.