Jumapili , 16th Mei , 2021

Ukiwa na passion na kitu chochote unaweza kukifanya na kufanikisha,hivyo kwa watu milioni 27.1 ya watanzania kuwa wanatumia internet unapaswa kujua utengeneze kitu gani ili uweze kupata soko.’

Hayo yameelezwa na Benson Shirima mbunifu kupitia Teknolojia wakati akihojiwa na EATV ambapo ameongeza kuna vijana wengi wamemaliza katika vyuo vikuu katika fani za ICT,na wamekaa tu nyumbani kwamba ajira hakuna lakini nchi ina mahitaji mengi yanayohitaji suluhu

''Mimi wakati nasoma,tukifanya malipo ya ada na malipo mengine tulikuwa tunatumia muda mrefu unatoka hapa na kwenda dirisha hili,wakati ingetumika mtandao utakaorahisisha kutoa huduma ingesaidia ni kama sasa malipo mengi ya serikali yanafanyika kwa mtandao,hii inaondoa urasimu na kupoteza muda.'' Benson Shirima mteknolojia wa Mtandao

Akizungumzia vikwazo ambavyo vijana wanakumbana navyo wakati wanataka kujiajiri kupitia Mtandao,anasema cha kwanza ni uthubutu,kuwa nikifeli itakuaje na ubinafsi miongoni mwa vijana.

Ameongeza kuwa ubinafsi huwakwamisha vijana katika kupiga hatua katika kuungana, mfano nina wazo langu na sitaki kushirikisha wengine,na nataka kutengeneza ufalme wa mtu mmoja,na pia kushirikiana na wengine siwezi kwa hofu ya kushika nafasi zetu,na hatuhitaji kuwa na wafalme wawili,haya yote hukwamisha vijana kusonga..