Jumamosi , 15th Feb , 2020

Jeshi la Polisi katika Mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza, Tabora, Shiyanga na kagera limefanikiwa kuwakamata watu zaidi ya mia tano wakijihusisha na masuala ya uhalifu pamoja na uganga wa jadi ambapo baadhi yao wanadaiwa kujihusisha na matukio ya ramli chonganishi.

Kubaka

Kukamatwa kwa watu hao ni kutokana na oparesheni maalumu iliyofanywa na jeshi hilo kufuatia agizo la Mkuu wa jeshi la polisi la nchini IGP Simoni Sillo, ambapo ilianza Febuari 3 mwaka huu, mbali na watuhumiwa vitu mbalimbali zikiwemo silaha za moto, matunguli ya waganga wa jadi na nyara mbalimbali za serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Geita Mkuu wa Oparesheni maalumu za jeshi la Polisi Nchini Kamanda Mihayo Msekela amesema pia wamemkamata Mganga ambaye alimtaka moja ya wateja wake kubaka wanawake 50 na kuwauwa ili apate utajiri lakini yeye aliwabaka 29.

Tazama video kamili hapo chini