Alhamisi , 19th Mar , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amepiga marufuku watu wanaojifanya kuwa ni madaktari na kuanza kutoa ushauri kupitia mitandao ya kijamii, kwani kwa kufanya hivyo inazidi kuleta taharuki na mkanganyiko kwa Watanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Sabaya ameongeza kuwa kipindi hiki ambacho Dunia inahangaika kukabiliana na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona ni vyema suala la utolewaji wa elimu likafanywa na wataalamu wa afya pekee.

"Madaktari wa Twitter, Instagram na Facebook tunawaomba katika hili muwapishe wataalam na Madaktari wa Binadamu wafanye wajibu wao!, mnachochangia zaidi katika hili ni confusion(mkanganyiko)!, suala hili linahusu maisha ya watu na sio siasa za bei rahisi" amesema DC Sabaya.