Ijumaa , 15th Feb , 2019

Jamhuri imempandisha kizimbani kijana, Emmanuel Mahumbi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuchapisha taarifa ya uongo katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu 'kichaa'.

Kesi hiyo ya jinai Na53 ya 2019 imeeleza kwamba Septemba 2018 mtuhumiwa alichapisha habari hizo katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.

Bw. Mahumbi aliandika kwamba, "Kichaa mmoja anatoa kafara kiboya kweli. Kaenda kumuona dada yake Bugando kumbe ndo anamkabidhi kwa Freemasons. Siku
moja baadaye ya akafa. Kaenda Ukerewe  siku mbili baadae wakafa. Kumbe alienda kuwakabidhi Freemasons. Boya kweli liambieni libadilike litamaliza watu,".

Bw. Mahumbi ameshtakiwa chini ya sheria za mitandao  (Cybercrime Act No4 of 2015)

Hata hivyo Wadau mbalimbali wameshangazwa na kitendo cha DPP kumfungulia mashtaka Bw. Mahumbi, ambapo Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amesema kwamba kwa kufanya hivyo, "Mahakama zitahemewa, magereza yatajaa sana".