Jumatano , 30th Sep , 2020

Mtu mmoja amefikishwa mbele ya Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es salaam kwa kosa la udanganyifu kwa kujifanya Afisa wa Polisi.

Mshtakiwa huyo, Joseph Vitalis,miaka 21 ambaye amefikishwa mbele ya Hakimu Sifa Jacob, na kusomewa mashtaka na wakili wa serikali Veronica Mtafya.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka,mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 21,2019 katika eneo la Tanganyika Packers jijini, Dar es salaam, kwa kujitambulisha kuwa ni afisa wa polisi Pc Mtaki mwenye namba J729 Jambo ambalo si kweli.

Hata hivyo baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa amekana kosa hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 12 mwaka huu.

Aidha Hakimu amesema kuwa dhamana iko wazi na mshtakiwa atatakiwa kusaini bondi ya shilingi laki tano na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi  wa Dar es salaam.