Alhamisi , 21st Nov , 2019

Wapenzi ambao ni wasanii wanaounda kundi la "Navy Kenzo" Aika na Nahreel wamesema hawajahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au bado, ila huwa wanaulizwa zaidi ndoa yao itakuwa lini.

Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo. Kulia ni Nahreel kushoto ni Aika

Wakipiga stori na EATV & EA Radio Digital Navy Kenzo, wamesema kwenye mahojiano yao mengi hawajawahi kuulizwa kama wamefunga ndoa au hawajafunga.

"Nyinyi mtajuaje kama ndoa haipo labda tumeshafunga, halafu hakuna mtu ambaye amewahi kutuuliza hilo swali, watu wanauliza ndoa lini labda kwa sababu hatujaweka mitandaoni ila kwaajili ya Watanzania tutatangaza hivi karibuni tutaweka tarehe na location" wamesema Navy Kenzo.

Wawili hao wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 10, tangu walipokutana chuoni nchini India, na wamebahatika kupata watoto wawili wa kiume ambao ni Gold na Jamaika.

Aidha kundi hilo la Navy Kenzo wamesema wataachia kazi zao mpya kwa mfumo wa "EP"  ambayo itaanza siku ya Ijumaa ya November 22.