Jumatano , 21st Aug , 2019

Hadi inafikia majira ya asubuhi ya Agosti 21, 2019 idadi ya vifo vya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro, imefikia 100 .

Hatua hiyo hiyo inakuja, baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,  kufariki usiku wa kuamkia leo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Hospitali ya Muhimbili Aminiel Aligaesha ,  amesema waliofariki ni Mazoya Sahani, Khamis Marjani na Ramadhani Magwila, na kusema kuwa majeruhi waliobaki ICU ni 13 na wawili wamelazwa wodi ya Sewahaji.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilipokea jumla ya majeruhi 47, ambapo hadi sasa, wamesalia majeruhi 15, huku wengine 32 wakiaga dunia.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10 katika eneo la Msamvu mkoani Morogoro  baada ya Lori la mafuta kuanguka na watu kujitokeza eneo la ajali, kwa nia ya kuchota mafuta na ndipo mlipuko wa moto ulipotokea na kusababisha majeruhi na vifo ambavyo hadi sasa vimefikia 100.