Jumapili , 10th Mar , 2019

Baada ya taarifa za ndege aina ya Boeing 737 ya Shirika la Ndege la Ethiopia ambayo ilikuwa na watu 157, kuanguka muda mfupi baada ya kupaa, na watu wote waliopo kwenye ndege hiyo kupoteza maisha, raia mmoja wa Tanzania ameeleza namna alivyopishana na ajali hiyo.

Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia

Kufuatia taarifa hiyo, Mtanzania, Antu Mandoza ambaye pia ni mjasiriamali wa urembo na tasnia ya habari, ameeleza namna alivyonusurika katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi ya leo.

Katika ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa alinusurika kukata tiketi katika ndege hiyo kabla ya kubadili safari ya Addis Ababa na baada ya kushuka ndipo alipokutana na taarifa hizo mbaya huku akipokea ujumbe mwingi na simu kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki waliotaka kujua hali yake.

 

Mwingine aliyenusurika na ajali ya ndege

 

Antonis Mavropoulos ambaye alizuiliwa kupanda muda mfupi kabla ya ajali ya ndege

Licha Antu Mandoza, mwingine aliyenusurika na ajali ya ndege hiyo ni, Antonis Mavropoulos raia wa Ugiriki ambaye amesimulia kuwa hakufanikiwa kuingia getini baada ya kuchelewa na iwapo angefanikiwa kuingia, angekuwa ni abiria wa 150 wa ndege hiyo.

Baada ya ajali kutokea alipelekwa kituo cha polisi cha eneo la Uwanja wa Ndege kwaajili ya mahojiano, ambapo maafisa wa Uwanja wa Ndege walifafanua kuwa walitaka kumhoji ni kwanini alikuwa ni abiria pekee ambaye hakuingia kwenye ndege hiyo.

Habari zilizothibitishwa na Shirika la ndege la Ethiopia zinasema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitoka Ethiopia kwenda Nairobi, na ilipata hitilafu angani na kupelekea kuanguka kwake.

Bonyeza hapa chini kusikiliza.