Jumatano , 22nd Jan , 2020

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa Tanzania itafanya uchaguzi huru na haki ifikapo Oktoba 2020, ambapo utakuwa uchaguzi wa kuwachagua Wabunge na Madiwani pamoja na Rais.

Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Mabalozi ambapo amesema atavialika vyombo vya uangalizi vya kimataifa kuja kuangalia uchaguzi huo.

"Mwaka huu Oktoba tutafanya Uchaguzi Mkuu na tumejipanga kufanyika kwa uhuru amani na haki, na wakati ukifika tutazialika nchi mbaimbali kuja kujionea namna Tanzania inavyokomaa kidemokrasia" amesema Rais Magufuli

Tazama video kamili hapo chini