Kushoto ni jinsi mkono wa Lemi Luchumi ulivyokatwa
Akizungumza na EATV amesema baada ya kupoteza mkono wake serikali ilimuondoa kijijni hapo kwa ajili ya usalama wake lakini baada ya muda alipaswa kurejea nyumbani ila kutokana na hali ya mazingira ya kijiji hicho bado anahofu na imemlazimu kuishi mji mdogo wa kibiashara wa Majimoto huku akikabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Akiendelea kutoa simulizi, Lemi amesema ana jumla ya watoto watano lakini kutokana na kukosa pesa ya kuwanunulia mahitaji muhimu ya shule watoto wake na kwa sasa amepoteza uwezo wa kufanya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.






